BOFYA "LIKE" KUUNGANA NASI

Cancel

HATARI: NYUMBA ALIYOIJENGA LULU YATUMIKA KWA KUTAPELI

Mjengo wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam umeingia kwenye lawama kufuatia madai kwamba, unatumika kwa kutapeli watu wanaotaka kununua nyumba maeneo hayo.
Mjengo wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kina makazi jirani na nyumba hiyo, baadhi ya watu wanaojiita madalali wamekuwa wakiwapeleka wateja kwa siri kwenye nyumba hiyo ambayo haijaisha na kusema inauzwa na Lulu mwenyewe.
MCHEZO ULIVYO
“Baadhi ya madalali feki wamekuwa wakiwaleta wateja wanaotaka kununua nyumba maeneo haya. Wakifika wanasema Lulu anaiuza, wakiwa wameshaiona wanatoa fedha za usumbufu au za kuwapoza wasipeleke watej wengine na kutoa namba feki ya Lulu ili mteja ampigie.

“Wapo wateja walishanifuata na kusema wanampigia Lulu hapatikani, lakini waliponionesha namba yenyewe si ya Lulu.

“Siku moja mteja mmoja aliletwa na dalali kuiona nyumba, akaipenda, akampa dalali shilingi 300,000 za kumfanya asipeleke wateja wengine, akampigia Lulu hakupatikana. Alipokuja kwangu nikaiangalia namba hiyo ilisajiliwa kwa jina la Mwanahamis nani sijui,” kilisema chanzo hicho.

MAPAPARAZI WAJIFANYA WATEJA, MADALALI WASHTUKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapaparazi wetu walijifanya wateja wa kuinunua nyumba hiyo na kwenda kukutana na watu wawili waliodaiwa kuwa ndiyo madalali, Kitwana na Mambeze ‘Mchopa’.

Baada ya mazungumzo, madalali hao walidai kuwa, funguo za kuingia ndani ya nyumba hiyo anazo mama Lulu (Lucresia Karugila) na alisema angefika siku hiyo saa kumi jioni na kuwataka mapaparazi kurudi muda huo.

Wakati mapaparazi wetu wanaondoka, dalali mmoja alisema: “Nyie kama mmekuja kututega mmeliwa wenyewe, hapa hakuna mtoto wa kijijini. Wanaokuja hapa kutaka nyumba wanajulikana, nyie mmetumwa.”

LULU ALISHAFIKA, HAJUI KITU
Sosi mwingine alisema hivi karibuni alimuona Lulu akifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia nyumba hiyo ambayo imesimama ujenzi lakini hakuweka wazi kama alikuwa na nia ya kuiuza!

“Mimi mara ya mwisho nilimuona Lulu eneo hili na gari lake, naona alikuja kuangalia nyumba inaendeleaje na usalama pia. Mambo ya kuwa anaiuza hata siyajui ingawa kweli hata mimi nimekuwa nikiwaona watu wakija,” alisema sosi huyo ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini.

Juzi, gazeti hili lilimsaka Lulu kwa njia ya simu kwa ajili ya kumuuliza kuhusu suala hilo ambapo, awali aling’aka, akasema:

“Wewe ndiyo unaniambia kusema ukweli, sijui chochote. Naomba mnipe habari kwa upana ilivyo maana nyie waandishi mara nyingi mnakuaga wa kwanza kujua habari kuliko mhusika.”

Amani: Wewe Lulu sema ukweli tu, kama unaiuza. Nilichokwambia ndicho.”

Lulu: Kweli mimi siiuzi nyumba yangu wala sina wazo. Huyo aliyewapa habari awape kwa undani ili nijue.”

»

VIDEO NA PICHA:HUYU NDIYE MWANAUME ALIYEJITOKEZA HADHARANI NA KUELEZEA ANAVYONYANYASWA NA MKE WAKE


Ndg Mustapha Manga

Super Woman Joyce Kiria

Je, umepata nafasi ya kufuatilia kisa hiki? Ni suala la kweli lililomkuta Mustapha ambaye analalamikia kuanyanyaswa na mke wake. Joyce Kiria na Wanawake Live tulipata nafasi ya kufuatilia kwa undani suala hili na hapa, pata sehemu ya kwanza na ya pili ya mazungumzo kati ya Super Woman Joyce Kiria na Mustapha kisha na mke wake Mustapha kufahamu mustakabali mzima wa familia hii.Mke wa Mustapha

Mke wa Mustapha wakijadiliana na Joyce Kiria

Je, baba Mustapha alipata alichokitaka? Ni nini hicho alichotaka? Tazama video hizi 3, na pia unaweza ukatembelea www.wanawakelivetv.com kwa ajili ya mengi zaidi.
Video 1: Mustapha »

MKE WA PETER WA P SQUARE AMETOA JIBU LA SHUTMA ZA KUSABABISHA UGOMVI WA KUNDI HILO..

Wakati mashabiki wa kundi la muziki linaloiwakilisha vizuri Afrika kidunia P-Square kutoka Nigeria wanaendelea kuwaombea ndugu hao wamalize tofauti zao, mke wa Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, amevunja ukimya kwa kuzungumza baada ya ripoti kumtaja kuwa sehemu ya chanzo cha matatizo ya familia hiyo yaliyojitokeza.
Kupitia ukurasa wake wa facebook Lola ambaye ni mama wa watoto wawili wa Peter ameandika:
“I’m a Lady of Substance though I have my Shortcomings, I might not be Loved by Everyone but the People that matters to me hold me in High Esteem and thats enough for Me.”
Peter Okoye na mkewake LolaKwa mujibu wa Naija Gists, chanzo kimoja kimesema ndugu hao wanafanya jitihada za kumaliza tofauti zao.

»

VIDEO:IKIRUKA KWENYE TV STATION ZA BONGO, TV HIYO LAZIMA IFUNGIWE FASTA KWANI NI CHAFU SANA

Mwanzoni ikiwa inaanza unaweza kusema kwamba ni ya kawaida, sasa cha kufanya jump hadi dakika 2 na sekunde 34 ambapo kwanza utakutana na warning ya Close your eyes then kinachofuata ni balaa.Msanii huyu anaitwa Maheeda maarufu kama bad girl wa Nigeria na video hii ina kick sana youtube hivi sasa lakini kwa uhakika haitachezwa kwenye vituo vya nchi nyingi sana.

»

LAANA ++SHOGA LAJINADI MTANDAONI NA KUWEKA NAMBA ZAKE ILI APATE WA KU DO NAE

www.facebook.com/brotherlucas

www.facebook.com/brotherlucas 
HAPA ALIKUWA ANAMNADI MWENZIE YAANI DUNIA ISHAHARIBIKA

»

MAPATO NA UTAJIRI WA IRENE UWOYA WAZUA UTATA

Inadaiwa kuwa hali ya hewa imechafuka kwa msanii nyota wa filamu za Bongo Irene Uwoya ambapo ameshindwa kutaja vyanzo vya utajiri wake wa Ghafla, Hivi karibuni Uwoya alikaririwa akisema kuwa hawezi kutaja kazi nyingine anayofanya na utajiri aliokuwa nao kwani wapo baadhi ya watu hawapendi kuona mmoja wao akiendelea ...Alisema kuwa pamoja na magari anayomiliki ya kifahari hawezi sema ni njia gani amepata utajiri huo..Nimefanya Filamu kadhaa ambazo zimenipa hela na cha zaidi ni Jina ambalo limenifanya kupata Deals zingine zinazonipa Pesa..Jina langu ni Kubwa so lazima liendane na Mali ninazopata...

»

SUNGUSUNGU LAWAMANI GEITA, WAMKAMATA MWANAMKE ALIYEVAA NGUO FUPI WAKAANZA KUMPAPASA MAKALIO KISHA KUMCHARAZA BAKORA


(picha ya maktaba)
****
Askari wa jadi maarufu kama sungusungu wa mtaa wa Mwatulole kata ya Kalangalala mjini Geita wanadaiwa kumdhalilisha na kumfanya ukatili mwanamke mmoja kwa kumkamata na kumcharaza viboko  kwa tuhuma za  kuvaa nguo fupi (kimini).

Inadaiwa kuwa walichukua uamuzi huo baada ya kamanda wao kuwaamuru na kutangaza sheria binafsi ya kuzuia watu kuvaa vimini kwenye mtaa huo.

Akizungumzia  kwa masitikiko mwanamke huyo, Jennifa Nobo (24) alidai kuwa alishambuliwa na sungusungu hao Aprili 15, mwaka huu katika mtaa huo wakati amekwenda sokoni.

Jeniffa alisema kuwa alipokwenda sokoni hapo kununua mahitaji ya nyumbani kwake, alikutana na sungusungu hao wakiwa wameongoza na kamanda wao huyo,  Daud Kulola.

Alidai baada ya kukutana nao, walimkamata, kumpapasa maungoni wa kumhoji sababu za kuvaa kimini ndani na juu khanga wakati kiongozi wao amepiga marufuku kuvaa mavazi hayo katika mtaa huo.

Jeniffer alidai bila kusikilizwa utetezi wake, sungusungu hao walianza kumcharaza viboko  hadharani na kumfuata kila alikokuwa akimbilia.

Alidai wakati wakicharaza viboko walimbakiza na kimini hicho. Aliendendelea kudai kuwa  kamanda huyo  alipochoka kumuadhibu, alimrejeshea khanga yake.

''Nlilipita kila kona akanifuata na kunicharaza kwa fimbo nililia sana na kutokwa na haja ndogo kwa  hofu na kipigo ..kilikuwa kitendo cha kinyama  ambacho  sijawahi kutendewa katika maisha yanguna,  sitakisahau, ''alidai..

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo walidai kuwa siku moja kabla ya tukio hilo la ukatili,  Kamanda huyo alisikiska akitumia kipaza sauti akitangaza kuwa  vijana na wasichana wote wake kwa waume wanaovaa vimini ni marufuku kuonekana mtaani.

Walidai wengi wao walidhani huenda lilikuwa ni agizo  la Serikali.

Baada ya tukio hilo Jeniffa alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Geita kufunguliwa jalada GE/RB/2033/ 2014 la shambulio la kudhuru  mwili kisha kupatia PF3 kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita.

Alisema baadaye polisi walimkamata kamanda huyo wa sungusungu na kuachiwa kwa dhamana na kwamba uchunguzi dhidi yake unaendelea.

Kamanda huyo alikataa kuzungumzia madai hayo dhidi yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo, Kalori Malicery amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukataa kuzungumzia kwa undani kwa madai limeripotiwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alionyesha kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kuzungumzia leo ofisini kwake.

Konyo alisema kuwa iwapo ushahidi utathibitika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.

»

MAPICHA YA POMBE SIO SUPU:ALEWA CHAKARI, ALALA STENDI

Vitabu vya Mungu vinataja kila kitu ni lazima kiwe na kiasi, ukizidisha basi kinachoweza kutokea ni aibu.
Jamaa mmoja ambaye jina halikupatikana mara moja, alijikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kunywa pombe na kulewa chakari na
Katika hali ya sintofahamu kijana mmoja amekutwa akiwa amelewa chakali na kulala kwenye stendi ya mwenge.
kukata ‘netiweki’ jambo lililosababisha ‘aangushe gari’ pembeni mwa stendi ya daladala ya Mwenge jijini Dar.
Ishu hiyo ilitokea wiki iliyopita ambapo paparazi wetu alibahatika kushuhudia laivu jamaa akijigeuzageuza kama yuko kitandani kwake.Kufuatia tukio hilo, kibaka mmoja aliamua kumgeuza dili mlevi huyo kwa kumsachi na kumchania mifuko yote ya suruali jambo Wananchi wakifanya jitihada za kumuamsha.
lililowaudhi waliokuwepo jirani na kumng’ang’ania mwizi huyo kutaka kumshushia kichapo.
“Samahani, msinifanye kitu chochote  sitarudia tena, nimefanya kosa sana, naomba mnisamehe ndugu zangu,’’ kibaka huyo alijitetea.

“Ushukuru Mungu tunakufahamu wewe, ila hujafanya kitendo cha kiungwana kabisa, unaweza kufa unajiona hivihivi, wewe si una
Akiwa hajiwezi kutokana na ulevi uliokithili.
nguvu?  Kwanini usifanye kazi kama wengine?’’ alihoji mmoja wa  watu waliotaka kumpiga kibaka huyo.
Mwandishi wetu aliamua kutafuta njia mbadala ya kumsaidia jamaa huyo wa gambe kwa kushirikiana na wasamaria wema ndipo maji

ya baridi yalipochukua nafasi kama huduma ya kwanza kwa kummwagia mwili mzima.
Baada ya kumwagiwa maji jamaa huyo alipata nguvu akaamka  na kuanza kuangaza macho huku na huko.

Hakuishia kufanya hivyo tu, aliinuka na kuanza kuondoka kwa kujikongoja lakini alipigwa butwaa baada ya kubaini mifuko yake yote ilichanwa kwa wembe.
Jamaa huyo alipoulizwa alikuwa akiishi eneo gani alijibu Ubungo, akapandishwa kwenye daladala iliyokuwa ikielekea huko.

»

NJIA SABA (7) ZA UHAKIKA ZA KUPATA AJIRA HIZI HAPA


Kupata nafasi za ajira imekuwa ngumu siku hadi siku, hususani ukitilia maanani kuwa wahitimu wanazidi kuwa wengi na hali ngumu ya uchumi inafanya waajiri kushindwa kuongeza nafasi mpya za kazi. Hauna haja ya kukata tamaa ya kupata kazi ile unayoitarajia hata kama kuna ukiritimba mwingi katika soko la ajira kama vile watu kupeana kazi kwa kujuana, nafasi za kazi kutotangazwa  au kazi haipatikani mpaka rushwa itembee. Makala hii inaenda kujadili mambo ya msingi kwa yeyote anayetafuta kazi, uwe kwa sasa umeajiriwa unatafuta kazi mbadala au uwe hauna ajira unatafuta ajira, bila shaka mambo tunayojadili hapa yatakusaidia.
1.Mtazamo wako kuhusu ajira:
Fahamu kuwa bidhaa ni chochote kile ambacho kinatimiza mahitaji fulani. Mwenye kuhitaji bidhaa huwa tunamuita mteja.  Muajiri anatafuta mfanyakazi kwa kuwa analo hitaji la kazi fulani kukamilika, na anayo matarajio kadhaa toka kwa mfanyakazi anayemuajiri.   Hivyo wewe kama mfanyakazi mtarajiwa unayo ‘bidhaa’, yaani uwezo wako wa kutimiza majukumu fulani ambayo utatakiwa kufanya na muajiri. Kwahiyo mtazamo sahihi unaotakiwa kuwa nao wakati unatafuta kazi ni kuwa wewe ni muuzaji wa bidhaa, na muajiri wako mtarajiwa ni mteja.  Kwakuwa wapo ‘wafanyabiashara’ wengi wa hiyo bidhaa kama yako (watu wanaotafuta ajira), unahitajika basi kujipanga vema ili kumshawishi na kumfanya mteja wako  (muajiri mtarajiwa) aone kweli sababu ya kununua ‘bidhaa ‘toka kwako.
2.Wasifu wako ujitosheleze:
Ukiwa na mtazamo tuliouleza hapo juu wa kuwa wewe ni mfanyabiashara unauza bidhaa kwa mteja wako (muajiri), unatakiwa basi utumie vema wasifu wako (CV) kujieleza vema ili ‘mteja’ akukubali.Mambo ya kuzingatia katika wasifu wako ni kama yafuatavyo:-

  • Wasifu wako uendane na aina ya kazi unayo omba: Hivyo basi usiweke kila aina ya maelezo hata yale ambayo haya umuhimu na kazi husika. Mfano unaomba nafasi ya kazi ya uhasibu, lakini unaweka maelezo ya uzoefu wa sehemu tatu tofauti ya kazi za ulinzi.
  • Wasifu wako uonyeshe kweli unao uwezo wa kazi unayoiomba:  Hivyo basi usitaje tuu majina ya kampuni au asasi ulizofanya kazi na aina ya cheo ulichoshika ukiwa huko, bali eleza mambo ya msingi ambayo  ni mafanikio ya wewe kuwepo katika kampuni au asasi fulani uliyokuwepo. Mfano kwa kazi yako kama msimamizi wa ofisi, uliweza andaa mikutano  (itaje) ambayo ilikutanisha watendaji wakubwa wa kampuni yako ambapo kupitia maandalizi mazuri uliyoyafanya, kampuni yako iliweza kupendekezwa mara tatu mfulululizo kuandaa mikutano hiyo.
  • Wasifu wako uonyeshe utofauti wako wewe na watu wengine: Haitoshi kuandika katika CV yako kuwa umemaliza masomo ya ngazi ya stashahada au shahada, haitoshi kutaja kuwa umewahi kufanya kazi fulani mfano kazi ya usimamizi wa ofisi halafu ukaorodhesha majukumu ya msimamizi wa ofisi, mambo ambayo kwa ujumla yanajulikana kuwa ni majukumu ya msimamizi wa ofisi yeyote yule wa ofisi. Kumbuka wasifu wako (CV) ni nyaraka muhimu ya kumshawishi ‘mteja’ kuwa ananunua ‘bidhaa bora zaidi ya nyingine katika soko la ajira. Hivyo basi jipange kwa kuonyesha utofauti, badala ya kutaja tuu ngazi za juu za elimu ulizofanikiwa kufika, taja pia maeneo ambayo wewe kweli ‘upo mzuri’ yaani maeneo ambayo kweli haubabaishi katika ngazi hizo za elimu unazotaja. Pia kwa upande wa uzoefu wa kazi, taja mafanikio uliyokwisha pata kutoka ajira zako zilizopita, au tuseme mambo gani ‘mazito’ ulikamilisha na kusaidia ukiwa kwa waajiri wengine.

3. Fuata maelekezo kwa ufasaha:  
Unapowasilisha maombi yako ya ajira, hakikisha unafuata maelekezo yaliyotolewa katika tangazo la nafasi za kazi, kwani hata kama ni jambo dogo, utakalokosea linaweza kuchukuliwa kama sababu ya wewe kutokuwa mfanyakazi makini, hivyo kukosa hata nafasi ya kuitwa kwa usaili (interview). Mfano kama umeambiwa uorodheshe wadhamini watatu, hauna sababu ya kuorodhesha wadhamini wawili tuu. Kama umeambiwa utume maombi kwa njia ya posta, usitume maombi yako kwa barua pepe wala kupeleka kwa mkono.Hakikisha pia unafuata maelekezo ya tarehe na muda wa kuwasilisha maombi yako ya kazi. Pia zingatia maelekezo kuhusu vyeti na nyaraka nyingine unazotakiwa kuziambatanisha pamoja na barua yako ya maombi ya kazi. Kama umeambiwa utume CV yako tuu, usihangaike kutuma vitu vingine kama vyeti, na barua ya maombi ya kazi.
4.Barua ya maombi ibebe uzito:
Barua yako ya maombi ya kazi ni nafasi nyingine ya kushawishi ‘wateja’ wako kuwa kweli utawapatia huduma wanayoitaka, na kwamba watakapofanya chaguo la kukuajiri wewe watakuwa wamefanya chaguo bora kabisa. Anza kwa kueleza aina ya kazi unayoomba, umetambuaje uwepo wa nafasi hiyo ya kazi. Jieleze kwanini wewe ni chaguo lao bora kwa kulinganisha majukumu ya kazi unayoomba na ujuzi wako, uzoefu wako, na yale uliyokwisha wahi kufanikisha hapo kabla.  Kwakuwa barua ya maombi ya kazi huwa ni fupi, usiwachoshe kwa maelezo mengi, ila maelezo yako yawavutie kusoma nyaraka ulizoambatanisha kama vile CV na  vyeti .
5. Jiandae kwa ‘interview’:
Utakapopata nafasi ya kuitwa kwa usaili, usiende bila kujiandaa. Fahamu vema majukumu yanayoendana na nafasi ya kazi uliyoomba, hakikisha unakumbuka nini uliandika katika barua yako ya maombi ya kazi na CV yako. Jikumbushe mambo ya msingi kuhusu elimu ya darasani ambayo umetaja unayo. Jifunze pia maswali mbalimbali ya kisaikolojia yaulizwayo katika usaili , kama vile ‘Tuambie madhaifu yako ni yapi ?”. Unaweza jifunza jinsi ya kujibu maswali kama hayo kupitia vitabu au hata kwa ku search kwa mtandao.
6. Usisubiri nafasi za kazi zikufuate:
Amini kuwa kuna waajiri wengi ambao hawatangazi nafasi za kazi kwenye vyombo vya habari au mitandaoni. Pia wapo ambao wamekwisha tangaza lakini hawajapata watu wenye kukidhi kweli viwango vyao. Hivyo usingoje nafasi za ajira zikufuate kwa kupitia vyombo vya habari, badala yake wewe mwenyewe wasiliana na waajiri mbalimbali ukiwaeleza nia yako na uwezo wako wa kufanya kazi kwao.  Waweza tembelea ofisi za makampuni au asasi mbalimbali na pia tembelea website  na hata maonyesho ya biashara au maonyesho ya waajiri (Job Fairs). Njia nyingine ni kujenga mitandao na watu mbalimbali ambapo kupitia mitandao hiyo waweza jieleza hitaji lako la kutaka ajira. Kumbuka kama una ‘bidhaa’ bora, na ukimpata mteja mwenye kuhitaji ‘bidhaa’, bila shaka una nafasi kubwa ya kupata ajira.
7. Itunze ‘taswira’ yako:
Waajiri wengi hupenda kufahamu zaidi kuhusu mtu wanayetaka kumuajiri, sio tuu uwezo wake kiujuzi wa kazi, bali pia uaminifu wako, wewe ni mtu wa aina gani katika kujiheshimu na kujiheshimu wengine n.k. Hivyo hakikisha hauharibu ‘taswira’ yako kupitia aina ya marafiki ulionao, aina ya twitts, status, picha n.k unazoweka katika mitandao ya kijamii kama Facebook, na Twitter. Pia unapotaka kuacha kazi toka asasi fulani , jitahidi uache kwa amani, isije baadae waajiri wako wengine wakataka kujua aina gani ya mfanyakazi ulikuwa hapo kabla wakajibiwa habari isiyopendeza

»

18+ MSANII CINDY WA UGANDA AACHIA PICHA ZA UTUPU KAMA ALIVYOZALIWA

Huyu ni yule Cindy msanii mkali wa Uganda aliyewahi kuwa member wa kundi la Blue 3 kabla hajaamua kufanya kazi kivyake. Kwa kweli ni aibu kwa msanii kama huyu kupiga picha kama hizi. YUKO UCHI KAMA ALIVYOZALIWA. NI AIBU SANA. 

»

KIONGOZI WA KANISA AMKINGIA KIFUA JOKATE....

KIONGOZI wa kwanya katika Kanisa la St. Peter, Oysterbay jijini Dar, Rogers Mgonja amemtetea mwanamitindo mahiri Bongo, Jokate Mwegelo kuwa hajalikacha kanisa kama inavyodaiwa.
Mwanamitindo mahiri Bongo, Jokate Mwegelo
Hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa, Jokate amezuiwa kutinga kanisani hapo kutokana na kuvaa mavazi ya nusu utupu yasiyoendana na maadili.
“Jokate ni mwanadada mwenye nidhamu sana kanisani, viongozi wote wanampenda ni mpole na msikivu, Kama ni mavazi, kanisani anavaa mavazi ya heshima ni ngumu sana kumfukuza kwa sababu ambazo haziingiliani na masuala ya kanisa,” alisema Mgonja.

»

VIDEO YA ALIJERUHIWA AKISIMULIA :CHID BENZ ALIVYOTAKA KUUA DEMU

Msanii wa Hip Hop anayetokea Ilala, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ amedaiwa kumpa kipigo kizito mpenzi wake wa zamani aliyefahamika kwa jina la Mwanaisha Kiboye.
Tukio hilo lililokusanya umati wa watu lilijiri Jumapili iliyopita maeneo ya Buguruni (kwenye mafleti) jijini Dar ambapo Chid alikuwa kwenye mizunguko yake na mpenzi wake wa sasa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
ISHU ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Chid na mpenzi wake huyo walifika katika baa moja maarufu iliyopo katika mafleti hayo na kumkuta Mwanaisha akiwa amekaa na rafiki zake. Demu huyo alimsalimia Chid na ndipo mtiti ukaibuka.
“Mwanaisha alipomuona Chid anakatiza na kwa kuwa aliwahi kuwa mpenzi wake, akaona siyo ishu bora ampe hai kwa mbali ndipo Chid alipomaindi na kumfuata huku akisema: unajifanya unanijua sana siyo? Ngoja nikuoneshe,” kilisema chanzo.

AMZIMISHA
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Chid kusema hivyo alimshushia kipondo kikali hasa sehemu za usoni na kumsababisha Mwanaisha achanike mdomoni kabla ya kuzimia palepale na kuanza kupepewa na marafiki zake, Chid akatokomea kusikojulikana.
Imeelezwa kuwa, Mwanaisha alipozinduka baada ya kupepewa alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Pangani, Ilala ambapo alipewa Fomu ya Polisi Nambari 3   (PF3) kisha kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu, Ilala - Amana.

CHID NAYE AKIMBILIA POLISI
Chanzo kimezidi kueleza kuwa, wakati Mwanaisha akianza kupewa matibabu hospitalini, Chid naye alishauriwa na marafiki zake kwenda kutoa taarifa katika kituo hicho cha polisi kama njia ya kujihami pasipo kujua kuwa  ameshawahiwa.
“Marafiki zake walioshuhudia tukio hilo walimshauri jamaa (Chid) akafungue mashitaka polisi kama njia ya kujihami, akakubali ndipo alipokwenda kutiwa nguvuni kwani tayari Mwanaisha alikuwa ameshamuwahi,” kilisema chanzo hicho.

ATUPWA MAHABUSU
Habari zimeeleza kuwa, Chid alipofika kituoni kwa ajili ya kutoa taarifa, alidakwa na kusokomezwa mahabusu kwa vile tayari alikuwa ameshafunguliwa mashitaka.
Chanzo kilichopo polisi hapo kimeliambia Amani kuwa, jamaa alipoambiwa avue mkanda ili atupwe sero alileta ubishi hivyo kusababisha polisi watumie nguvu ya ziada kumdhibiti kwa sababu alisema yeye ni mtu maarufu hivyo hawawezi kumtisha.

AKUTWA NA BANGI
Wakati msanii huyo anayesifika kwa  sauti nzito akitaka kuingizwa ndani, alisachiwa na kukutwa na misokoto miwili ya bangi hivyo kuandikishwa kesi nyingine ya madawa ya kulevya mbali na ile ya awali ya kujeruhi.

MWANAISHA ANASEMAJE?
Juzi Jumanne, Amani lililimsaka Mwanaisha ambapo lilifanikiwa kumkuta nyumbani kwao, maeneo ya Sharifu Shamba,  Ilala akiwa hawezi kutembea, kuongea vizuri akiwa hoi kitandani.
Akizungumza kwa shidashida, Mwanaisha alisema anasikitika kuona Chid amempiga bila kisa.
“Sijui hata kwa nini aliamua kunipiga, amenipiga vibaya, nimeshonwa nyuzi 12 na bado nasikia maumivu makali kichwani,” alisema.
Kwa mujibu wa dada wa Mwanaisha ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, watafuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo ili kuona mwisho wake kwani mbali na kumweka majeraha ndugu yake lakini bado hali ni mbaya na wanatakiwa kumfanyia Kipimo cha CT Scan.
“Hizi gharama zote tutakazohangaika kumtibu ndugu yetu lazima Chid azilipe maana amempiga ndugu yetu pasipo kufanya kosa lolote,” alisema dada wa Mwanaisha.

APANDISHWA KIZIMBANI
Kwa kuwa Jumapili na Jumatatu ilikuwa Sikukuu ya Pasaka, juzi Jumanne Chid alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo - Ilala na kusomewa mashitaka mawili; KUJERUHI na KUKUTWA NA BANGI.
Siku hiyo, mahakama ilimsomea mashitaka na kutakiwa kujibu kama ni kweli amefanya makosa hayo lakini mshitakiwa huyo alikanusha makosa yote mawili hivyo kesi hizo kuahirishwa.

KESI ZATOFAUTISHWA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mahakama hiyo, kesi ya kujeruhi inatarajiwa kutajwa tena mahakamani hapo Aprili 24, mwaka huu (leo) huku ile ya kukutwa na bangi ikisogezwa mbele hadi Mei 6, mwaka huu.

APATA DHAMANA
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hizo, mshitakiwa alipewa nafasi ya kupata dhamana kwa masharti ya kulipia shilingi 100,000 huku akidhaminiwa na watu wawili ambapo Chid alitimiza masharti hayo na kuachiwa huru kusubiri kesi zitajwe tena.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Ilala, ACP Marieta Minangi amekiri kutokea kwa tukio hilo.

»

SIKILIZA:STORI JUU YA MSANII LINEX KUKOSWA KUPIGWA RISASI...

Hii imetokea Mwanza ambayo inamhusu Linex kukoswa kupigwa risasi na mtu asiyemfahamu hii imetokea Mwanza baada ya kuwa ametoka hotelini kwenda kwa washkaji zake,ambapo katika harakati za mabishano ndipo jamaa akatoa bunduki. 88.1 Clouds Fm inasikika ukiwa Mwanza.
Bonyeza play kusikiliza.»

HIVI NDIVYO TATOO HII YA DINI INAVYO MSUMBUA MTALII HUYU

mtaliiUnaambiwa Mtalii mmoja raia wa Uingereza amekataliwa kuingia nchini Sri Lanka baada ya kupatikana akiwa na Tattoo ya dini ya Budhaa kwenye mkono wake.
Naomi Michelle Coleman alikamatwa na maafisa wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada ya maafisa wakuu kuiona Tattoo hiyo kwenye mkono wake wa kulia.
Tafsiri ya dini hiyo kulingana na Budhaa mwenyewe inasemekana alikuwa mtu mwenye busara na hekima kubwa na pia mwanzilishi wa dini hiyo ambayo mafunzo yake mengi yalijenga msingi wa dini yenyewe.
Msemaji wa polisi amesema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini ambapo Hakimu aliamuru Bi.Coleman kurejeshwa nchini kwao.
Kwa sasa amezuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao na inasemekana Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.
budhaaBi Coleman aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bandaranaike siku ya Jumatatu kutoka nchini India ambapo maafisa baada ya kuiona Tattoo hiyo ya Budhaa akiwa amekaa kwenye mauwa walimkamata.
Kwenye kumbukumbu Mwezi Machi mtalii mwingine muingereza, alizuiwa kuingia katika uwanja huo baada ya maafisa kusema kuwa alijibu kijeuri alipohojiwa kuhusu Tattoo aliyokuwa amechorwa ambayo pia ilikuwa na Budhaa.
Source:Bbc.

»

PICHA 8:HANDAKI LA AJABU LAONEKANA ENEO LA KITANZINI IRINGA.

 
Umati wa watu waliofika katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo

mkuu wa Wilaya Ya Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa nyumba ambayo handaki hilo limeonekana
Handaki lenyewe muonekano wa sehemu ya kuingilia
Mkuu wa Wilaya kushoto aipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazio wa kampuni ya maji Iringa
Handaki la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema lake Mtandao huu ulipokutana na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu yakuridhisha huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi. Handaki hilo ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza katika kuchimba ndipo walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na kudhani kuwa inatumika kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo. Akizungumza mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kufahamu kilichopo. Ameeleza kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani. Anazidi kueleza kuwa walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza kuendelea kutokana na kuzibwa. mkuu wa Wilaya afika eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio huku akiwa na wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa wa usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo. nini maoni ya wakazi waliofika katika eneo hilo? Wengi wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote.

»

UJIO MPYA WA OMMY DIMPOZ BAADA YA TUPOGO, CHEKI VIDEO YA WIMBO MPYA

Ommy Dimpoz a.k.a Poz kwa poz ameamua kuwaonjesha kionjo cha wimbo wake mpya unaokuja ambao video yake imefanywa nchini Marekani Na producer mkali nchini humo. Kupiti Account yake ya Instagram Ommy dimpoz aliweka kionjo cha Video hii na kusema ndio cha wimbo huo unaosubiriwa na Wapenzi wa Muziki wa Bongo fleva Kwa Hamu Kubwa.


Sikiliza Na kumtazama Hapa:»

HUU NDIO UJUMBE WA DIAMOND PLATNUMZ WA KUSISIMUA ALIOMUANDIKIA MADEE

10251451_379012242238325_1980205357_n
Ikiwa leo ndio kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake raisi wa Manzese, Madee. Tarehe 25 mwezi kama huu, wasanii mbali mbali wametokea kumtakia maisha marefu na wengine kumpongeza kwa njia mbali mbali, ila kwa hii ya Diamond Platnum ni kali kuliko yote, Diamond ameamua kushusha ya kwake yamoyoni kupitia account yake ya instagram, katika kukubali juhudi zake, kama msanii mkongwe na kumshukuru kwa yote.
f9a90b92ca9111e382ce0002c999ad18_8
“Naamini moja ya kitu kinachokufanya uzidi kufika mbali na kufanikiwa zaidi ni jinsi ulivyo na upendo kwa wasanii wote.. hususan upcoming, Nimenza kukuskia kabla sjui lini nami ntakuwa flani hadi leo kufikia hapa lakini skuzote umekuwa ukinisuport tangu naanza hadi sasa na kunielekeza katika kazi zangu mbalimbali… Nakuheshim sana Bro! Happy birthday.. Mungu akupe maisha maref yenye amani na mafanikia tele… Eta Tudele!” alimalizia Diamond Platnumz

»

TANESCO NJOMBE WANASA WEZI WA NYAYA ZA UMEME KITUO CHA MKOA HUO

 Shirika la Umeme Tanesco Wilaya ya Njombe Leo Limefanikiwa Kuwanasa Watu Wawili Waliokutwa Wakiiba Nyaya za Umeme Katika Kituo cha Kusambazia Umeme Yaani Power Station Mjini Njombe Huku Wawili Wakihusika Katika Tuhuma Tofauti Ikiwemo Ya Kununua Nyaya Hizo na Mmoja Kushindwa Kuwajibika Kama Mlinzi wa Zamu.
Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Nne Asubuhi Huko Katika Mtaa wa Uzunguni Kwenye Kituo Hicho cha Umeme Yaani Power Station Ambapo Vijana Wawili Wamekatwa na Mmoja Ametokomea Kusiko Julikana Wakati Wa Msako Huo.

Akizungumza Mara Baada ya Kuwafikisha Kwenye Kituo cha Polisi Mjini Njombe Msimamizi wa Shirika la Umeme Wilaya ya Njombe Bwana Renatus Henerico Amesema Kuwa Wizi wa Nyaya Hizo Ulianza Tangu Wiki Iliyopita Lakini Kutokana na Kuweka Mtego wa Kuwanasa Wezi Hao Leo Zoezi Hilo Limefanikiwa.

Bwana Renatus Amewataja Watuhumiwa Hao Kuwa ni Pamoja na Justin Kyando Mwenye Umri wa Miaka 17 Mkazi Wa Ramadhani Mjini Njombe,Gehazi Kilumbe Mwenye Umri wa Miaka 18 Ambaye naye ni Mkazi wa Mtaa Huo wa Ramadhani,Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Nyaya Hizo Pamoja na Anna Mhenga Ambaye Alikuwa Mlinzi wa Zamu Katika Lindo Hilo.

Aidha Amemtaja Castory Mligo Kuwa Ametoroka wakati Wa 
Tukio Hilo na Kwamba Miongoni Mwa Vijana Hao Wawili Walikuwa Wafanyakazi wa Mkataba Mfupi Katika Shirika Hilo Yaani S.T.E Ambapo Baada ya Mkataba Wao Kuisha Wakaanza Kujihusisha na Matukio Hayo.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Nyaya Hizo Zilizo Ibiwa Hadi SasaZinagharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni 60 Kwani Walianza Kuiba Tangu Siku Nyingi.

Blog hii Imefanikiwa Kuzungumza na Mmoja wa Watuhumiwa Hao Anayefahamika Kwa Jina la Justin Kyando Ambaye Amesema Kuwa Wamekuwa Wakiiba Nyaya Hizo naKuziuza Kwa Mfanyabiashara Huyo Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Vyuma ChakavuKatika Mtaa wa Msichoke Mkabala na Chuo Kikuu cha Amani Mjini Njombe.


Bwana Christian Mlelwa ni Mkuu wa Ulinzi Katika Kampuni Ya Jirani Security GroupYenye Makao Makuu Yake Jijini Dar es Salaam Ambaye Amesema Amekuwa Akimuomba 

Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Kumuongezea Walinzi Hususani Katika Eneo Hilo la PowerStation Lakini Hakuna Utekelezaji Wowote Kwani Eneo Hilo ni Kubwa Zaidi.

»

SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA: LULU AMEANZA YALE YALE YA ZAMANI YALIYOMPOTEZEA DIRA..

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
  Kwako Elizabeth Michael ‘Lulu’. Leo nimeona nikukumbuke kupitia barua! Natambua uwezo wako mkubwa katika kazi, juhudi zako binafsi ndiyo zimekufikisha hapo ulipo, mataifa mbalimbali sasa wanatambua kuwa kuna mtu anaitwa Lulu, yupo Bongo, muigizaji!.

Sitaki kukurudisha sana nyuma lakini najua unajua kuwa ni jinsi gani kipindi cha nyuma ulikuwa ukipamba vyombo vya habari kwa skendo chafu. Ulipoteza dira ya kimaisha, watu wengi waliokuwa wakikufuatilia kazi zako walianza kukutupa.
Walikupotezea kwa sababu ya matukio ya ulevi, mavazi ya nusu utupu na matukio mengi ya ajabuajabu yaliyofanana na hayo. Sina nia mbaya kukumbusha lakini waswahili wanasema binadamu anajifunza kutokana na makosa. Maishani mwako umekutana na mazito yasiyofanana na umri wako.
Kwenye ulimwengu wa mahaba, ilikuwepo minong’ono mingi juu ya watu wanaotajwa kushiriki mapenzi na wewe, walitajwa vigogo, mastaa na hata wasio mastaa. Sitaki kusema ni kweli au la lakini lisemwalo kama halipo, ujue laja.
Siri ilifichuka kupitia kifo cha yule unayedai alikuwa mwandani wako, marehemu Steven Kanumba.
Mazingira ya kifo chake, umri mdogo uliokuwa nao ilikuwa ni fundisho kubwa maishani mwako. Ulipambana na msalaba wa gereza, ukapambana na mlolongo wa kesi mahakamani hadi pale ulipofanikiwa kutoka kwa dhamana, Januari mwaka jana.
 
Baada ya kutoka mahabusu, kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa ulikuwa kimya, ulionekana kubadilika kitabia. Yale uliyokuwa ukiyafanya awali, uliyaweka pembeni na zaidi kusimamia mustakabali mzima wa maisha yako, ulikuwa mwema sana aisee!. Kinachonisikitisha ni kuanza kusikia tena matukio ya ajabu, unaonekana kubadilika. Nimefuatilia tabia zako, naona umeanza kubadilika, umesahau eeeh! Mavazi yako kwa miezi michache iliyopita, nimegundua yanaanza kuchepuka! Mfano mzuri ni kigauni ulichokivaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe yako ya kuzaliwa. Hakikustiri maungo yako nyeti, kilionesha sehemu kubwa ya matiti yako.
Kama hiyo haitoshi, kupitia mitandao ya kijamii umeanza kushusha matusi mazito bila sababu za msingi, mtu akikukosoa kidogo, unampa maneno machafu ambayo hayaandikiki gazetini. Kama kioo cha jamii, unapaswa kuvumilia mengi.
Nikiwa kwenye kazi zangu za kila siku, huwa nakuwa wa kwanza kupata fununu za mabadiliko ya kila msanii na namna anavyoishi. Nikuonye tu, kuwa makini na mwenendo wako kwani tayari jamii ilishaanza kujenga imani na wewe. Uliaminika na ndiyo maana ukapata bahati ya kuchukuliwa katika kampuni nzuri ikakusimamia kazi zako hadi sasa. Kwa kuwa tayari nimeanza kupata malalamiko kutoka katika vyanzo vyangu, nikusihi sana mdogo wangu, usirudi ulipotoka. Jenga heshima mpya na jamii ikuamini kutokana na kazi zako na si skendo za ajabuajabu, kwa leo ni hayo tu!
Wasalam.
Ni mimi Anko Erick Evarist.
-GPL

»

ISABELA NA KALAMA WAMWAGANA....

Ule uchumba wa muda mrefu wa wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda an Kalama Bakari ‘Luteni’ umevunjika kwa kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa uaminifu baina yao.
Wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda 'Bella' na Kalama Bakari ‘Luteni’ wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Global TV Online hivi karibuni  kabla ya kumwagana.
Chanzo makini kilicho karibu na nyota hao wawili, kilisema kuachana kwao kunatokana na Luteni Kalama kukosa uaminifu kwa mwenzake kwani mara kadhaa, Isabela alizifuma meseji za wanawake wengine kwenye simu yake.
Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ memba wa Kundi la Gangwe Mobb katika pozi.
Kana kwamba haitoshi, Kalama ambaye ni memba wa Kundi la Gangwe Mobb, pia hivi karibuni, licha ya kutotokea kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Isabela, lakini alishindwa hata kumtumia ujumbe wa kumtakia heri.
“Ni kweli nimeamua kujiweka pembeni kwa sababu Kalama siyo mwaminifu, nilikuta meseji mbalimbali za mapenzi za wanawake wengine, naogopa Ukimwi, bora nikae pembeni nimuache aendelee kufanya umalaya wake maana huyu ni sikio la kufa,” alisema Isabela baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi wa habari hizo.
“Kilichoniumiza zaidi, hivi karibuni ilikuwa bethidei yangu hata hajani-wish kunijulia hali wakati nilikuwa ninaumwa, bora niendelee na maisha yangu, ndiyo maana mmeona hata kwenye uzinduzi wa Global Tv kila mtu alikuja kivyake.”
Kalama alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Mimi sijui kama tumeachana, lakini kama Isabela ameamua hivyo ni sawa tu, ninachojua kila mtu yupo kwake, mimi niko Tabata yeye Kijitonyama.”

»

WACHINA WAMZOMEA:JACK PATRICK AANGUA KILIO KORTINI..

HATIMAYE modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.
Kete zinazosadikiwa kukutwa na modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ akiwa amezimeza.
Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia.

Jack akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kunaswa.
“Yeye alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu,” kilisema  chanzo chetu.
Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu.

Jack akiwa karibu na madawa aliyonaswa nayo.
KUNA MADAI ALIZOMEWA
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.

Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara, inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.

“Unajua ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana,” kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.
Jack Patrick.
KAMA ATARUDI BONGO SALAMA
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005, aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama atabahatika kurejea Bongo salama,

atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya nchi.
TUJIKUMBUSHE
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha unga huo.

Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’ kukutwa imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi waliliona si la kawaida kwa msichana kama yeye.

»